Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amewapongeza wachezaji wake kwa ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa KMC Complex jana
Akikiongoza kikosi cha Yanga katika mechi ya pili, Hamdi aliwashuhudia vijana wake wakicheza soka la daraja la juu na kuwapoteza kabisa wapinzani wao
Kama Yanga ingetumia kila nafasi kwa usahihi pengine wangefunga zaidi ya mabao 10 katika mchezo huo
""Napenda kuwapa pongezi Wachezaji wangu leo wamecheza katika kiwango cha juu sana, wote tumeshuhudia walivyojituma na kufanya mashambulizi wakati wote tofauti na mchezo wetu uliopita na huu ndio mpira ambao mashabiki wetu wanataka kuuona na kuufurahia katika kila mechi tutakayocheza"
"Yanga ni timu kubwa sana, ina wachezaji bora mno. Mchezo tulionesha leo ni hadhi ya ligi ya mabingwa. Tumecheza mpira mkubwa sana. Nimeridhika mno na jitihada za vijana wangu. Kwa namna tulivyocheza leo tumedhirisha ukubwa wetu," alisema Hamdi
Hamdi ameshuhudia ushindi wa mabao 6-1 mara mbili katika mechi tatu tangu alipotua Yanga
Mechi ya kwanza dhidi ya KenGold alishuhudia ushindi kama huo akiwa jukwaani
Kikosi chake sasa kinakwenda kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Singida BS siku ya Jumatatu katika dimba la KMC Complex