Mshambuliaji Clement Mzize anaongoza mbio za ufungaji bora msimu huu akiwa na mabao 9
Baada ya mechi za raundi ya 18 kukamilika, Mzize yuko pale juu akifunga mabao yake bila mikwaju ya penati
Ukiangalia orodha ya vinara 6 wa ufungaji, ni Prince Dube pekee mwenye mabao 7 ambaye nae hana bao la penati
Elvis Rupia wa Singida BS, Lionel Ateba na Jean Ahoua wote wa Simba ambao wamefunga mabao 8, wana mabao ya mikwaju ya penati
Ateba ana mabao 4 ya penati, Ahoua ana mabao 3 na Rupia ana bao 1
Pacome Zouzoua wa Yanga nae yuko katika orodha hiyo akifunga mabao 7, moja likiwa la mkwaju wa penati
Dube na Mzize ndio wanaotegemewa katika safu ya ushambuliaji ya Yanga msimu huu huku Pacome akiendeleza makali yake pia
Nyota hawa wanapigiwa chapuo katika mbio za kuwania ufungaji bora