FT : JKT Tanzania 0-0 Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Feb 2025
FT : JKT Tanzania 0-0 Yanga, NBC PL

Yanga imeshindwa kutamba uwanja wa Isamuhyo baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Yanga ilitengeneza nafasi chache katika kipindi cha kwanza Clement Mzize akikaribia kuifunga lakini umahiri wa mlinda lango wa JKT Tanzania ulikuwa kikwazo

Kipindi cha pili JKT Tanzania walirudi nyuma kuzuia huku wakitumia mashambulizi ya kushitukiza

Licha ya jitihada, haikuwa rahisi kuipenya ngome ya JKT na kushuhudiwa dakika 90 zikimalizika ubao ukisoma 0-0

Unaweza kusema Yanga haikuwa katika 'form' yake leo, ilijenga mashambulizi yake taratibu hivyo kuwapa JKT Tanzania nafasi ya kujipanga

Yanga inaendelea kubaki kileleni ikifikisha alama 46 hata hivyo kama Simba itashindi dhidi ya Tanzania Prisons hapo kesho, maana yake ni kuwa mabingwa hao watetezi watashuka nafasi ya pili

Ni mchezo wa kwanza msimu huu Yanga inadondosha alama ugenini baada ya kushinda mechi zote 7 zilizopita

Dimba la Isamuhyo bado ni gumu kwa Yanga kupata ushindi, matokeo kama haya yalipatikana msimu uliopita pia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’