Moallin ampa maua yake Ramovic

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Feb 2025
Moallin ampa maua yake Ramovic

Licha ya kutimkia CR Belouizdad, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic, ametajwa kushiriki maandalizi ya timu hiyo iliyopata ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya KenGold FC katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam juzi

Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Abdihamid Moallin ambaye alikaimu nafasi ya Kocha Mkuu katika mchezo huo, alisema ushindi huo ameupeleka kwa Ramovic

Moallin alisema hauwezi kuutengenisha ushindi huo na Ramovic kwa sababu walikuwa wote hadi dakika ya mwisho katika maandalizi

"Kwanza niwapongeze wachezaji wangu wamefanya kazi kubwa sana, ushindi huu wa mabao sita naupeleka kwa kocha mwenzangu, Ramovic, huwezi kumtenganisha na mafanikio haya, tulifanya naye kazi kubwa katika maandalizi ya mchezo huu, kutengeneza mfumo na kuwasoma wapinzani wetu"

"Kwa hiyo hizi pointi tatu na ushindi huu na yeye pia anahusika ameingia katika rekodi hii. Kwa maana hiyo namzawadia yeye," alisema Moallin

Aliongeza matokeo ya ushindi mnono yametokana na kufanyia kazi mapungufu waliyobaini katika mechi iliyotangulia dhidi ya Kagera Sugar

"Tulipoteza nafasi nyingi katika mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar hasa kipindi cha kwanza, tukapata bao moja tu, lakini katika mchezo huu 'tumeua' mechi mapema, tumefunga mabao manne kipindi cha kwanza, hii inaonyesha wachezaji wangu wamekifanyia kazi kile tunachowaelekeza pamoja na mapungufu yaliyojitokeza," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’