Wakati Yanga ikichezeshwa na waamuzi 7 tu katika mechi zao 16, timu ile imechezeshwa na waamuzi 11!
Lakini la kushangaza zaidi ni kuwa Yanga inachezeshwa na wale waamuzi ambao wanaaminika ni bora na wana beji za FIFA
Ahmed Arajiga ndio kinara wa kuchezesha mechi za Yanga akichezesha mechi nne huku Aly Mnyupe akifuatia akichezesha mechi tatu
Hakuna mechi ya timu ile ambayo Arajiga amechezesha wala mwamuzi yeyote aliyechezesha mechi za Yanga
Sasa unajiuliza huyu Arajiga ambaye anaaminiwa na CAF akichezesha mechi za Ligi ya Mabingwa, kombe la Shirikisho na hata kufuzu michuano ya Afcon, hajapewa mechi hata moja ya timu ile?
Inashangaza sana pale malalamiko juu ya waamuzi yanapokuwa mengi hasa katika mechi za timu ile lakini mwamuzi bora zaidi Tanzania kwa sasa Arajiga hapewi mechi zao?
Angalia waamuzi 11 waliochezesha mechi za timu ile, miongoni mwa mwao ni kinamama watatu Amina Kyando, Tatu Malogo na Ester Adarbert ambao wamelalamikiwa mara kadhaa lakini pia Shomari Lawi na Kefa Kayombo hawa ndio vinara wa kuchezesha mechi za timu ile licha ya kuwa nao wamelalamikiwa mara kadhaa
Hapa mamlaka zinapaswa kuzinduka maana yaonekana kuna dalili za upangaji matokeo nje ya uwanja
Timu ile mechi zao hawapewi wanaoaminika kuwa waamuzi bora badala yake inapewa wale waamuzi ambao wamelalamikiwa sana juu ya uchezeshaji wao
Waamuzi hao wengine hupewa mechi moja moja tu na pale wanapokuwa wamekamilisha lao hawapewi mechi nyingine! Wakati huo tayari 'makosa yao ya kiubinadamu' yameipa faida timu ile
Ndio maana utaona timu ile waaamuzi wanaochezesha mechi zao ni wengi kwani akitumika mmoja katika mechi nyingi, itabainika anawabeba