Ligi Kuu ya NBC inarejea leo baada ya kipindi cha mapumziko, mabingwa watetezi Yanga wakishuka uwanjani kuikabili Kagera Sugar. Ni katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex, saa 10 jioni
Hii ni mechi ya kiporo ya raundi ya 16 ikiwa pia ni mechi ya kwanza kwa Yanga katika duru la pili
Baada ya kushindwa kupenya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa, kwa sasa Yanga inaelekeza nguvu zake zote katika michuano ya ndani, Ligi Kuu na kombe la Shirikisho la CRDB
Malengo ya Yanga ni kutetea nataji yote hayo ambayo wanayashikilia kwa misimu mitatu mfululizo
Hivyo ni wazi leo Wananchi wanahitaji matokeo ya aina moja tu, ushindi ili kuwaondoa watani zao Simba juu ya msimamo wa ligi kabla ya mchezo wao dhidi ya Tabora United hapo kesho
Lakini ni wazi mchezo huo hautakuwa mwepesi, Kagera Sugar ni miongoni mwa timu zenye kawaida ya kuipa Yanga changamoto kila zinapokutana licha ya Yanga kuwa na takwimu bora dhidi ya wapinzani wao hao
Kagera Sugar inashika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi, wakiwa na alama 11 tu. Hii ni aina ya mechi ambayo watacheza kana kwamba hakutakuwa na mechi nyingine
Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic anakwenda kukiongoza kikosi chake katika mechi ya 6 ya ligi akiwa ameshinda mechi zote 5 zilizopita
Tangu Wananchi walipohamia dimba la KMC Complex, hawakamatiki kwani wameshinda mechi zote walizocheza katika uwanja huo huku wakifunga angalau mabao 3 katika kila mchezo
Itakuwa mechi ngumu lakini ni wazi Kagera Sugar watahitaji kuwa bora pengine kuliko wakati mwingine wowot ili kuondoka na chochote katika mchezo huo