Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar yanaendelea vizuri
Jana Yanga ilifanya mazoezi katika uwanja wa KMC Complex kuelekea mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, Februari 1
Walter amesema ukimuondoa Yao Kouassi, wachezaji wengine wote wamerejea mazoezini na wako tayari kwa mchezo huo
"Kila kitu kinaenda vizuri, tumekuwa na maandalizi mazuri tangu mchezo uliopita. Kikosi kimetimia kwa maana wachezaji wote (isipokuwa Yao) wapo kamili kuelekea mchezo huo"
"Kocha ana uwanja mpana wa kuchagua nani ataenda kuiwakilisha Yanga siku ya Jumamosi, hilo ni jambo zuri kwetu"
"Niwaombe mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi siku ya Jumamosi kutuunga mkono katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar"
"Mashabiki wa Yanga siku zote wamekuwa sehemu ya mafanikio ya timu yao kwani wanajitokeza kwa wingi uwanjani iwe tunacheza hapa Dar es salaam, mikoani na hata nje ya nchi"
"Tunawashukuru kwa sapoti yao wakati wote na tunawaomba waendelee kuwa nasi," alisema Harrison
Chini ya kocha Sead Ramovic Yanga imekuwa na rekodi ya ushindi wa asilimia 100 katika ligi
Wananchi wanahitaji kushinda dhidi ya Kagera Sugar matokeo ambayo yatawapeleka kileleni mwa msimamo wa ligi