Pacome aahidi ubingwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jan 2025
Pacome aahidi ubingwa Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua amewapa pole mashabiki wa timu hiyo baada ya timu yao kushindwa kufuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Pacome amesema hata wachezaji wameumizwa na matokeo hayo lakini sasa wameweka ahadi kuhakikisha wanatetea mataji yote wanayoshikilia ili kurejea katika michuano hiyo wakiwa imara zaidi msimu ujao

"Kuna wakati unaona ni kama ndoto kukosa kucheza robo fainali, kuna wakati unapata matokeo ambayo yanashtua, hii imewaumiza sana mashabiki wetu na hata sisi wachezaji"

"Haitakuwa nzuri kama tutawaumiza na kukosa makombe ya ndani ambayo tunayashikilia, tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunatetea makombe yetu yote," alisema Pacome ambaye aliugua malaria siku chache kabla ya mchezo dhidi ya USM Alger lakini akaomba apewe nafasi katika mchezo huo ambao aliingia kipindi cha pili

Wikiendi hii Yanga itaanza safari ya kutetea taji la Kombe la FA itakapoikaribisha Copco kutoka Mwanza, mchezo wa hatua ya 64 Bora utakaocheza Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam

Baada ya mchezo huo, Februari 1 Yanga itaanza mechi za duru ya pili ligi kuu ya NBC kwa kuikabili Kagera Sugar katika mchezo utakaopigwa dimba la KMC Complex

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’