Tutafute dawa ya kutumia vyema uwanja wa nyumbani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jan 2025
Tutafute dawa ya kutumia vyema uwanja wa nyumbani

Katika moja ya maeneo ambayo uongozi wa Yanga unapaswa kufanyia kazi, ni kutengeneza hofu kwa wapinzani hasa timu inapocheza katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kwa mara nyingine jana Yanga imeshindwa kutumia vyema uwanja wa Benjamin Mkapa kufuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya MC Alger

Ni mchezo ambao Yanga ilihitaji kushinda ili kufuzu lakini dakika 90 hazikutosha kuwapa Wananchi ushindi katika ardhi yao

Msimu huu Yanga imekusanya alama nne pekee nyumbani, ikishinda 3-1 dhidi ya TP Mazembe na kupoteza 2-0 dhidi ya Al Hilal

Kutotumia vyema uwanja wa nyumbani ni kilio cha Wananchi kwa miaka mingi pengine jambo hili sasa linapaswa kutengenezewa mkakati ili kuhakikisha Yanga inaongeza ufanisi inapocheza nyumbani katika mashindano ya CAF

Kama mechi ya MC Alger jana ingekuwa ni ugenini pengine Yanga ingeweza kushinda! Katika misimu ya karibuni Yanga imejenga tabia ya kufanya vizuri ugenini kuliko nyumbani kulikoni?

Hata katika msimu wa 2022/23 ambao Yanga ilicheza fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC), katika hatua ya mtoano ilishinda mechi zote ugenini lakini ikakosa ushindi nyumbani kwenye mechi ya kwanza ya fainali dhidi ya USM Alger halafu ikashinda mechi ya pili Algeria katika mchezo ambao uligubikwa na figisu za kila aina

Uongozi wa Yanga unapaswa kuona kama hili ni tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka

Kwa utamaduni soka la Afrika, uwanja wa nyumbani ndio eneo la kujidai ukienda ugenini huko lolote linaweza kutokea

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’