Matchday : Al Hilal vs Yanga, CAF CL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jan 2025
Matchday : Al Hilal vs Yanga, CAF CL

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wako uwanjani huko Mauritania kumenyana na Al Hilal katika mchezo wa raundi ya tano hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Hii ni mechi muhimu kwa Yanga kushinda ili kuweka hai matumaini ya kuwania kufuzu robo fainali ya michuano hiyo

Ni wazi itakuwa mechi ngumu, lakini kwa Yanga hakuna matokeo mengine yanayohitajika zaidi ya ushindi

Kama Yanga itapoteza mchezo huo maana yake itakuwa imekubali kuyaaga mashindano hayo

Akizungumzia hali ya kikosi kuelekea mchezo huo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo, ari na morali ya timu ikiwa juu

"Tumekuwa na maandalizi mazuri hapa Mauritania, niseme tu ukiangalia nyuso za wachezaji, wanakuonyesha dhamira ya kutaka kushinda mchezo huu dhidi ya Al Hilal"

"Kila mmoja anafahamu kama tutakosa ushindi basi tutakuwa tumejiweka katika mazingira magumu ya kufuzu au kuondoshwa katika michuano kama tutapoteza kabisa"

"Tunafahamu ubora wa Al Hilal, tutakwenda kupambana nao kwa dakika zote 90 na kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi," alisema Kamwe

Mchezo huo utapigwa saa 4 usiku kwa saa za Tanzania ambapo huko Mauritania itakuwa saa 1 usiku

Kila la kheri Wananchi....!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’