Tutapambana kusaka ushindi dhidi ya Al Hilal - Ramovic

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jan 2025
Tutapambana kusaka ushindi dhidi ya Al Hilal - Ramovic

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema mpango wa mchezo dhidi ya Al Hillal uko wazi kwani wanahitaji kuibuka na ushindi ili kuweka hai matumaini ya kufuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Ramovic alisema wamejipanga na watajaribu kila linalowezekana ili kushinda mchezo huo mgumu ugenini

Ramovic amebainisha kuwa kikosi chake sasa kiko katika kiwango bora tofauti na walivyocheza na Al Hilal katika mchezo wa kwanza uliopigwa Dar es salaam hivyo matarajio yake utakuwa mchezo wenye ushindani

"Katika miezi michache iliyopita, tumepiga hatua kubwa na tumekuwa bora zaidi. Haya ni matokeo ya kile tulichofanya, na kile tunachoendelea kufanya"

"Hatutaki kuwa wa kwanza kupoteza nafasi dhidi ya wapinzani wetu. Kimsingi, tutajaribu kila kitu kesho ili kuona kama tunaweza kufanikisha lengo letu, tunajua kwamba jambo muhimu ni ushindi na tunalichukulia kwa uzito mkubwa"

"Mpango wetu uko wazi, tunapaswa kuonyesha kwamba tunaweza kupata magoli na kushinda. Tunacheza dhidi ya timu yenye nguvu kubwa katika eneo la ulinzi kwa hiyo tunapaswa kuwa wabunifu kesho na kujaribu kutumia nafasi zetu vizuri zaidi"

"Tunapaswa kuonyesha ukuaji wetu, tuchukue kila nafasi kwa umakini na tuwe na uthubutu wa kushambulia ili tuweze kutengeneza nafasi ya ushindi. Wanacheza kwa kasi na tunapaswa kuwa tayari kukabiliana nao," alisema Ramovic

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki amesema watacheza kwa bidii kubwa hapo kesho ili kupata matokeo mazuri mbele ya Al Hilal

"Kwa niaba ya Wachezaji wenzangu kwa upande wetu tuna lengo moja na lengo hilo ni kuendelea kwenye hatua inayofuata. Ili kufanikisha hilo, tunapaswa kucheza kwa bidii zaidi kesho hili ni jukumu letu na tutafanya kila kitu kuhakikisha tunafanikiwa," alisema Aziz Ki

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’