Kikosi cha Yanga tayari kiko Mauritania kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa Jumapili, Januari 12 katika uwanja wa Cheikha Boidiya
Mtanange huo utakaopigwa saa 4 usiku utaamuliwa na waamuzi kutoka Rwanda
Mwamuzi wa kati ni Samuel Uwikunda ambaye atasaidiwa na Dieudonne Mutiyimana na Didier Ishimwe huku mwamuzi wa nne akiwa Rurisa Fidele
Katika mchezo huo, Yanga inahitaji ushindi wa aina yoyote ili kuweka hai tumaini la kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo
Yanga yenye pointi nne kwa sasa ikishika nafasi ya tatu, ilipoteza mbele ya vinara hao wa Kundi na timu pekee iliyofuzu robo hadi sasa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mabao 2-0 zilipokutana jijini Dar es Salaam
Msimu huu Yanga haikuanza vyema hatua ya makundi kwani kwenye mechi tatu imekusanya pointi nne dhidi ya Mazembe ilipotoka sare ya 1-1 na kuichapa nyumbani mabao 3-1, ikipoteza dhidi ya Al Hilal na MC Alger kwa mabao 2-0