Mechi ya kuamua hatma ya Yanga CAF CL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jan 2025
Mechi ya kuamua hatma ya Yanga CAF CL

Wawakilishi pekee wa nchi katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga Jumamosi wanakabiliwa na mechi ngumu ya ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DR Congo), itakayochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam

Mechi hiyo inaweza kuamua hatma ya Yanga kuvuka kwenda hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya kimataifa

Meneja wa Habari na Mawasliano wa Yanga, Ali Kamwe, alisema wamekaa na wachezaji na kukubaliana mechi ya kesho watacheza kama hakuna mchezo mwingine watakaocheza tena kwa sababu ndio utakuwa daraja la wao kwenda hatua mbele ya michuano hiyo, vinginevyo watakuwa wamejiweka katika hali mbaya

Kamwe alisema wakati wachezaji wakihamasishana 'kufia uwanjani' katika mechi hiyo, amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuwashangilia na kuwapa hamasa na kuufanya Uwanja wa Benjamin Mkapa uwe kama 'tanuri la moto' kwa wapinzani

Alisema haipendezi kwa klabu kama Yanga ambayo msimu uliopita ilifika hatua ya robo fainali ishike mkia katika kundi kutokana na kuvuna pointi moja pekee baada ya kucheza michezo mitatu

TP Mazembe ilitua nchini mapema jana tayari kwa ajili ya mchezo huo wa raundi ya nne, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 mjini Lubumbashi, hapo Desemba 14, mwaka jana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’