Msafara wa TP Mazembe unatua leo nchini kuelekea mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumamosi, Januari 04 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Wakati Mazembe wakitua leo, kikosi cha Yanga kinakamilisha maandalizi ya mchezo huo ambao utaamua hatma ya Yanga katika michuano hiyo msimu huu
Katika salamu zake za kuukaribisha mwaka 2025, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said aliweka bayana kuwa malengo ya Yanga kwa mwaka huu ni kushinda mataji yote ya ndani pamoja na kufika hatua za juu zaidi katika michuano ya ligi ya mabingwa
Sare ya bao 1-1 waliyopata dhidi ya Mazembe katika mchezo wa kwanza uliopigwa Lubumbashi, ilirudisha uhai wa Yanga katika michuano hiyo
Yanga sasa itahitaji ushindi katika mechi ya mkondo wa pili Jumamosi ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali