Zoezi la usajili limekamilika kwa asilimia 95

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
28 Jul 2017
Zoezi la usajili limekamilika kwa asilimia 95
leo Yanga imemalizana na kiungo mkabaji Papi Kabamba Tshishimbi ambaye jana alifuzu vipimo vya afya. Amepewa mkataba wa miaka miwili.

Yanga pia imemuongeza mkataba wa miaka miwili mshambuliaji Matheo Antony.

Aidha kwa upande wa nafasi moja ya mchezaji wa Kimataifa iliyobaki, mmoja wa wajumbe wa kamati ya usajili ametuhakikishia kuwa Mnigeria Henry Tony Okoh ndiye atasaini mkataba baada ya kupendekezwa na benchi la Ufundi.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Yanga, Hussein Nyika amesema zoezi la usajili sasa limekamilika kwa asilimia 95.

Aidha ametuhakikishia kuwa Yanga iko mbioni kukamilisha usajili wa kiungo wa Mbeya City Raphael Daudi na huenda mambo yakawa sawa wikiendi hii.

Ikumbukwe dirisha la usajili linafungwa rasmi Agosti 06.

Wakati huo huo Nyika amesema Yanga imefanya usajili madhubuti wenye lengo la kuhakikisha inafanya vizuri kimataifa.

Nyika amesema kwa kuwa Yanga haina mpinzani kwenye soka la Tanzania, msimu ujao imejipanga kun'gara zaidi Kimataifa.

"Kamati imefanya kazi kubwa, Yanga inalenga kuliteka soka la Afrika na si hapa nyumbani tu. Wanachama wa Yanga waondoe hofu kuhusu timu yao," amesema Nyika

Nyika ameahidi kuachia lileeee bomu Jumapili ijayo.

Nenda kwenye ukurasa wa Videos umsikie Nyika akiahidi kuhusu bomu hilo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’