Gusa achia twende kwao itawaacha salama Fountain Gate?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Dec 2024
Gusa achia twende kwao itawaacha salama Fountain Gate?

Ni saa chache zimebaki kuelekea mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Fountain Gate ambao utapigwa saa 10 jioni katika uwanja wa KMC Complex

Utakuwa ni mchezo wa tano kwa kocha Sead Ramovic katika ligi ambapo nne zilizopita ameshinda zote dhidi ya Namungo (2-0), Mashujaa (3-2), Tanzania Prisons (4-0) na Dodoma Jiji (4-0) huku ushindi wa mabao 4-0 mfulululizo ukiwapa jeuri zaidi.

Baada ya kukiongoza kikosi chake kwa takribni wiki nne, Yanga sasa imeamka ikitandaza soka safi ambalo linaweza kuwafanya Fountain Gate kupoteana mapema leo kama hawatakuwa imara

Katika kutengeneza mashambulizi yake kuhakikisha wanapata ushindi, Ramovic amekuwa akipata jeuri kubwa kupitia Prince Dube kwani katika mabao 13 yaliyofungwa chini ya kocha huyo ligi kuu, yeye amehusika mara saba akifunga matano ikiwemo hat trick moja na asisti mbili.

Mbali na Dube, Clement Mzize naye amekuwa vizuri kwani hadi sasa amefunga mabao matano, wakati Pacome Zouzoua akiwa mkali wa asisti akiongoza kikosini hapo akifikisha nne na kufunga mabao matatu.

Si eneo la ushambuliaji pekee ambalo limekuwa na kazi ya kufunga, bali hata beki Ibrahim Hamad ‘Bacca’ naye ni mwiba mchungu kwa wapinzani kutokana na kufunga mabao manne.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari jana, Ramovic alisema anatarajia mchezo huo utakuwa mgumu kwani Fountain Gate sio timu nyepesi lakini dhamira yao ni kuona wanaibuka na ushindi

"Tumejiandaa na mchezo huu kama tulivyojiandaa na mchezo uliopita, tunawaheshimu wapinzani, tumewaangalia wapinzani ni wagumu sana, tunachohitaji ni kwenda kuchukua pointi tatu"

"Ili kupata ushindi lazima upambane kwelikweli, huwezi kushinda kirahisi. Hatuangalii kilichopita, kilichopo mbele yetu ni cha muhimu zaidi," alisema Ramovic

Meneja wa habari na mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema mechi hii ina umuhimu wa kipekee kwa sababu ni mechi ya mwisho mwaka 2024

Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao ambapo leo watashangilia kwa kutumia kauli mbiu ya 'Gusa, achia twenda kwao'

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
31m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
40m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’