Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga leo wanarudi uwanja wa nyumbani, KMC Complex kuikaribisha Fountain Gate
Ni mechi ya kufunga mwaka 2024, Wananchi pia wakifunga hesabu za duru la kwanza kwa kukamilisha mechi ya 15
Yanga ni kama imejipata chini ya kocha Sead Ramovic na bila shaka Fountain Gate leo watahitaji kufanya kazi ya ziada kupata chochote katika mchezo huo utakaopigwa saa 10 jioni
Gusa, achia twende kwao ya Yanga imeanza kusumbua, Wananchi wakipachika mabao 13 katika mechi 4 zilizopita huku wakiruhusu mabao mawili tu
Yanga iko katika nyakati bora wachezaji wakianza kuzielewa mbinu za 'Germany Machine' kwa kucheza soka la kasi na kufanya 'pressing'
Yanga inazihitaji alama tatu za mchezo dhidi ya Fountain Gate ili kuendelea kuwapa presha watani zao Simba katika mbio za ubingwa