Kila mchezo una maandaizi tofauti - Ramovic

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Dec 2024
Kila mchezo una maandaizi tofauti - Ramovic

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema amepata muda wa kutosha kukiandaa kikosi chake kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate utakaopigwa Jumapili Disemba 29

Akizungumza katika Mkutano na wanahabari, Ramovic amesema amewasoma Fountain Gate na kukiandaa kikosi chake kwa kuzingatia aina yao ya uchezaji kwani anatambua kila mchezo unahitaji mbinu tofauti

"Tumepata Muda mzuri wa kujiandaa na tayari tumewasoma Wapinzani wetu, Kiukweli ni Wapinzani Wagumu lakini kwa ukubwa wa timu hii pamoja na maandalizi yetu, tupo tayari kujitoa kwa asilimia mia moja ili kukusanya alama tatu"

"Kila Mchezo huja na Maandalizi tofauti, kwakuwa malengo yetu kesho ni kushinda basi tumejiandaa kucheza mchezo mzuri na kutengeneza nafasi za kutupa Alama tatu"

"Hatutatazama kabisa matokeo ya mechi zilizopita, za kwetu pamoja na za kwao, Sisi tunautazama mchezo huu kwa umakini mno, niwaombe Wananchi waje kutusapoti siku ya kesho kwasababu tunawahitaji sana," alisema Ramovic

Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji

Ramovic ameiongoza Yanga katika mechi nne za ligi na kushinda zote. Alianza na dozi ya mabao 2-0 dhidi ya Namungo Fc kisha dozi hiyo kuongezeka katika mechi zilizofuata

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
32m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’