Tumejiandaa kwa mechi ngumu dhidi ya Dodoma Jiji - Ramovic

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Dec 2024
Tumejiandaa kwa mechi ngumu dhidi ya Dodoma Jiji - Ramovic

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema kikosi chake kiko tayari kwa mechi ngumu ya ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambayo itapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma

Akizungumza katika Mkutano na wanahabari, Ramovic alisema ameichambua Dodoma Jiji na kubaini ni timu ngumu hasa inapocheza katika uwanja wa Jamhuri hivyo watahitaji kucheza kwa tahadhari kubwa ili kupata alama 3

"Tumewatazama kwa makini sana Dodoma Jiji, wanacheza vizuri wakiwa nyumbani, tunafahamu ni wagumu mno wanapocheza nyumbani hivyo tumeshajiandaa kukabiliana nao. Alama tatu kesho muhimu mno kwetu ili tuendelee kubaki kwenye mipango yetu"

"Ushindi katika mchezo huo unabeba dhima nzima ya kujitoa kwa kila namna, kama tusipojitoa kwa kila hali hapo kesho matarajio ya ushindi yatakuwa madogo"

"Kimsingi tumekuja hapa na tumeshajiandaa kisawasawa na tuna imani ya kuondoka alama tatu. Bila shaka mchezo umekaa kimtego kutokana na ratiba lakini hiyo haiondoi dhamira yetu ya kushinda," alisema Ramovic

Aidha kocha huyo raia wa Ujerumani amesema atalazima kufanya 'rotation' ya kikosi cha katika baadhi ya nafasi ili kuhakikisha anatunza nguvu ya kila mchezo kwa ajili ya mapambano katika mechi ambazo zinafuatana karibu karibu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’