Nyota Yanga wafurahia 'come-back' ya Dube

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Dec 2024
Nyota Yanga wafurahia 'come-back' ya Dube

Mshambuliaji Prince Dube ameshaliamsha balaa baada ya kutupia kwa kasi tena akianza na hat trick kwenye ligi, hatua ambayo imekuwa faraja pia kwa mastaa wenzake ndani ya kikosi hicho wakisema jamaa atafunga sana.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, nahodha msaidizi wa Yanga beki Dickson Job amesema kwamba kila mmoja ndani ya kikosi hicho alikuwa anasubiria nyakati kama hizi kuona Dube anaonyesha makali yake kwa kufunga mabao.

Job alisema Dube ni mshambuliaji mwenye uwezo na akili kubwa anayejua kujipanga kwenye nafasi za kufunga na ndio maana walikuwa wanampa moyo kwa kujua kufunga kwake ni suala la muda tu.

"Hakuna asiyejua makali ya Dube ndio maana yupo katika klabu hii kubwa kwani ana akili kubwa sana ya mpira na kipaji kikubwa, lakini katika soka inatokea kuna wakati washambuliaji wanakutana na wakati mgumu kama hiki alichokutana nacho," alisema Job

"Unajua sio kwamba alikuwa hafungi, kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa tulimuona anafunga ilikuwa imebaki kufunga katika ligi tu, tukiwa mazoezini pia alikuwa anafunga vizuri ila kwenye mechi mnamuona anapata shida"

"Tulichokuwa tunafanya ni kumtia moyo kwamba aendelee kupambana na sio yeye tu hata wengine huwa tunawapa moyo kwa kuwa tunajua wana uwezo, kwenye timu tunashirikiana kwa kuwa sisi wote tunapigania lengo moja sasa naona mabao yamerudi ni hatua kubwa kwake na timu yetu kwa ujumla," Job alinukuliwa na Mwanaspoti

Wakati Job akisema hayo kiungo wa timu hiyo, Pacome Zouzoua alisema anaamini mabao ambayo Dube ameyafunga juzi dhidi ya Mashujaa yatamrudishia hali ya kujiamini na kufunga mabao mengi zaidi.

Pacome alisema kasi ya Dube katika timu yao ina umuhimu mkubwa ambapo inawarahisishia wao kama viungo kutoa pasi kwa wakati mwafaka.

"Ukiangalia bao ambalo nilimtengenezea alikimbia kwa wakati sana na akajiweka sehemu ambayo mabeki hawakushtuka. Kasi yake ni kitu bora sana, tuna washambuliaji wenye kasi sana hata Mzize (Clement) Musonda (Kennedy)"

"Nadhani sasa atakuwa anaendelea kufunga mabao zaidi kwa kuwa ile hali ya kujiamini itakuwa imerejea kwa nguvu ni mshambuliaji mwenye juhudi na anajua kufunga," alisema Pacome

Baada ya ukame wa mabao kwa muda mrefu, Dube sasa amefunga mabao manne katika mechi mbili zilizopita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’