Tathmini ya kikosi kuelekea mchezo dhidi ya Mashujaa Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Dec 2024
Tathmini ya kikosi kuelekea mchezo dhidi ya Mashujaa Fc

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic leo anakwenda kukiongoza kikosi chake katika mchezo wa pili wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc katika uwanja wa KMC Complex

Ni mechi muhimu kwa Yanga kushinda ili kuhakikisha inapunguza gap la pointi dhidi ya timu zilizo juu yake lengo likiwa kurejea kileleni mwa msimamo

Ramovic anakwenda katika mchezo huo akiwa na kikosi chake imara licha ya kuwa baadhi ya wachezaji wanaweza kukosekana kutokana na sababu mbalimbali

Taarifa rasmi iliyotolewa na Yanga jana ilithibitisha kukosekana kwa Clatous Chama ambaye anauguza jeraha la kiwiko cha mkono

Bila shaka Stephane Aziz Ki leo atarejea katika kikosi cha kwanza baada ya kutoanza mchezo uliopita wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe

Mlinda lango Djigui Diarra huenda akapumzishwa na Aboubakar khomein kukaa langoni

Diarra alipata majeraha katika mchezo dhidi ya TP Mazembe, kulingana na taarifa iliyotolewa na msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, afya yake imeimarika lakini ana asilimia 50 za kucheza kama ilivyo kwa mlinzi wa kushoto Chadrack Boka

Pengine habari njema zaidi kwa mashabiki wa Yanga ni kurejea kwa Clement Mzize katika safu ya ushambuliaji

Mzize alicheza dakika 45 za mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe na kuonyesha kiwango kizuri

Bila shaka Ramovic leo hatasita kumuanzisha Mzize katika kikosi chake cha kwanza, anaweza kumtumia kama winga au mshambuliaji wa kati

Ramovic hatarajii kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake, pengine nyota wengi walioanza katika mchezo uliopita dhidi ya TP Mazembe, watatumika leo

Hii ni mechi muhimu kwa Yanga kushinda ili kuendelea kurejesha ari na morali ya timu kabla ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Januari 03 2025

Mechi hizi nne zinazofuata za ligi kukamilisha duru ya kwanza ni muhimu kwa Yanga kushinda zote. Pia ni maandalizi mazuri kuelekea mchezo dhidi ya Mazembe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’