Nkane awaita mashabiki kwa wingi KMC Complex

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Dec 2024
Nkane awaita mashabiki kwa wingi KMC Complex

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Denis Nkane amesema wachezaji wanatambua ugumu wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc ambao utapigwa uwanja wa KMC Complex hapo kesho lakini watahakikisha wanaibuka na ushindi

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake kuelekea mchezo huo, Nkane amewataka mashabiki wa Yanga wajitokeze kwa wingi dimba la KMC Complex kushuhudia mchezo huo huku akiahidi ushindi

"Sisi wachezaji tunafahamu Mashujaa ni aina ya timu ambayo imekuwa na matokeo mazuri katika uwanja wao wa nyumbani na hata ugenini"

"Hivyo tunafahamu tunakwenda kukutana na mchezo mgumu, lakini alama tatu kwetu ni muhimu. Tumeshajiandaa kwa namna yoyote watakavyokuja"

"Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi uwanja wa KMC Complex kutuunga mkono katika kuipigania nembo ya klabu yetu,"alisema Nkane

Kesho Yanga ni kama itakuwa inazindua uwanja wa KMC Complex kwani itakuwa mara ya kwanza kwa mabingwa hao wa nchi kucheza katika uwanja huo baada ya kuhama Azam Complex

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’