Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema kiwango cha utimamu wa kimwili cha wachezaji wake kilikuwa chini sana na amelazimika kufanya kazi kubwa katika uwanja wa mazoezi
Ramovic amesema ni jukumu la kila mchezaji kujituma ili kuwa bora na kwa wale ambao hawawezi kwenda na msimamo huo, haoni kama wanastahili kuendelea kuitumikia Yanga
"Baada ya mazoezi ya wiki tatu sasa nimeanza kuwafahamu vyema wachezaji wangu ubora na madhaifu yao"
"Tmu hii inasimamia katika nidhamu, uwajibikaji na kujituma. Hiki ndicho wachezaji wa timu hii wameonyesha katika misimu mitatu iliyopita ma kushinda mataji yote ya ndani na kucheza fainali ya CAF CC na robo fainali ya CAF CL"
"Sasa tuna nafasi ya kuona ni mchezaji gani yuko tayari kutwaa ubingwa kwa mara nyingine na mchezaji gani ameridhika na mafanikio ya misimu iliyopita. Kila mchezaji atakuwa na nafasi kuonyesha kile alichonancho"
"Na kama nilivyosema tangu mwanzo tunahitaji wachezaji ambao wako 'fit' na ukweli ni kwamba bado hatuko katika 'fitness' ambayo tunapaswa kuwa. Lakini sio tatizo kwa sababu tunaweza kuboresha hili"
"Ni lazima tufanye kazi kubwa katika uwanja wa mazoezi, kila mchezaji anapaswa kuonyesha anataka kuimarika kinyume chake huyo mchezaji yuko katika klabu ambayo hapaswi kuwa"
"Sijui kilitokea nini huko nyuma lakini ukweli ni kuwa nilipokabidhiwa timu hii kuna wachezaji hawakuwa 'fit' kabisa. Kuna wachezaji hawako katika utimamu unaotakikana na ndio maana unaona tulipata shida katika baadhi ya mechi"
"Lakini wanaweza kuimarika kama wanataka, kama hawataki nafikiri ni sahihi kusema wanapaswa kutafuta timu nyingine za kucheza"
"Ili kushinda mechi ni lazima wachezaji wawe 'fit',ni lazima wafahamu kile wanapaswa kufanya uwanjani, wawe 'compact', ni lazima wakimbie pamoja kushambulia na kurudi nyuma kuzua pamoja. Kama hatufanyi hivyo tutaacha nafasi kati yetu na kuwapa mwaanya wapinzani wetu kuzitumia," alisema Ramovic