Ligi Kuu ya Wanawake inaendelea leo ambao kinadada Yanga Princess watakuwa wenyeji wa JKT Queens katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex
Ni mechi muhimu kwa Yanga Princess kuzisaka alama tatu ili kupunguza gap la pointi kati yake na JKT Queens na Simba Queens ambazo ziko juu ya Wananchi katika msimamo
Yanga Princess imekusanya alama 9 katika nafasi ya tatu huku JKT Queens wakiwa nafasi ya pili na alama 14 na Simba Queens wakiongoza na alama 16
Ili Yanga Princess iwe na matumaini ya kuendelea kuwania ubingwa msimu huu, inahitaji ushindi leo ili angalau kusogea karibu ya washindani wake

ADVERTISE HERE