Ni saa chache zimesalia kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa saa 10 jioni huko Lubumbashi, DR Congo
Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic leo anaelekea katika mchezo huo akiwa na kikosi imara mbacho huenda kikajumuisha wachezaji ambao hawakutumika katika mchezo uliopita
Kiungo Khalid Aucho leo anaweza kurejea kikosini baada ya madaktar wa Yanga kujiridhisha amepona kabisa majeraha na yuko tayari kuipambania Yanga
Lakini pia Dickson Job na Clement Mzize nao wako timamu na pengine leo wanaweza kushuhudiwa wakiipigania Yanga katika dimba la TP Mazembe
Beki Chadrack Boka alishiriki mazoezi ya mwisho jana lakini pengine hajakuwa na fitness ya kutosha na inaweza kuwa hatari kumuanzisha katika mechi ngumu ambayo Yanga inahitaji ushindi
Ukitoa wachezaji hao, Ramovic atakuwa na nyota wake wote aliowatumia katika mchezo uliopita ambao Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya MC Alger
Hakutarajiwi kuwa na mabadiliko makubwa katika kikosi chake kitakachoanza mchezo wa leo
Benchi la ufundi limewaandaa wachezaji wote kikamilifu, kila mmoja anafahamu umuhimu wa mchezo dhidi ya Mazembe leo
Jambo jema ni kuwa kila mchezaji anaonyesha kuwa tayari kuipigania nembo ya Yanga jioni ya leo
Bila shaka Yanga itarejesha tabasamu katika nyuso za mashabiki wake baada ya kuanza vibaya ligi ya mabingwa msimu huu