Boka afufua matumaini ya kuikabili TP Mazembe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Dec 2024
Boka afufua matumaini ya kuikabili TP Mazembe

Jana baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi walishiriki kikamilifu mazoezi ya kwanza Lubumbashi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe utakaopigw kesho Jumamosi

Miongoni mwa wachezaji hao ni mlinzi wa kushoto Chadrack Boka ambaye alionekana mara ya mwisho uwanjani Novemba 02 katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao hata hivyo hakuweza kumaliza dakika 90

Katika mechi mbili za ligi ya mabingwa ambazo Yanga ilipoteza dhidi ya Al Hilal na MC Alger, Nickson Kibabage alitumika nafasi ya Boka lakini Wananchi wengi hawajaridhishwa na ufanisi wake katika eneo hilo

Pengine ndio sababu Yanga imemsajili Israel Mwenda ili kuongeza nguvu katika eneo hilo hasa Boka anapokosekana

Hata hivyo Mwenda bado hajasajiliwa kwa ajili ya kuitumikia Yanga katika ligi ya mabingwa dirisha la usajili la CAF litafunguliwa Januari 1 2025.Pia ataanza kutumika katika mechi za ligi kuu baada ya kusajiliwa pale dirisha la TFF litakapofunguliwa Jumatatu, Disemba 16

Wachezaji wengine ambao wamerejea kikosini baada ya kupona majeraha ni Khalid Aucho, Dickson Job na Clement Mzize

Yanga leo itakamilisha maandalizi katika uwanja wa Mazembe, pengine baada ya mazoezi hayo hatma ya nyota hao kuelekea mchezo wa kesho itafahamika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’