Nyakati ngumu hupita - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Dec 2024
Nyakati ngumu hupita - Kamwe

Licha ya kupoteza mchezo dhidi ya MC Alger juzi, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki na wanachama waendelee kuiunga mkono timu yao kwani bado wanayo nafasi ya kufanya vizuri katika mechi zilizobaki

Yanga ilifungwa mabao 2-0 na MC Alger ukiwa ni mchezo wa pili mfululizo mabingwa hao wa Tanzania Bara wanapoteza na kujikuta wakiburuza mkia kundi A

Kamwe amekiri Yanga inapita katika nyakati ngumu lakini ni vyema kuendelea kuwa na imani huku wakiwaunga mkono viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wao kwani anaamini nyakati kama hizi hupita

"Hayakuwa matokeo rafiki na hatukujiandaa nayo, huwezi kwenda kwenye michuano mikubwa kama hii ukiwa na mategemeo ya kupoteza, lengo letu lilikuwa kushinda, lakini ndiyo maisha ya mchezo wa mpira wa miguu, ziko nyakati nzuri na zipo nyakati ngumu, sisi kama Yanga tunakiri sasa tupo katika nyakati ngumu"

"Tumeona hata Manchester City nayo haifanyi vizuri, inapitia kwenye wakati mgumu, kikubwa ni kurudi tena imara, haitakiwi hali hii kuendelea," alisema Kamwe

Β "Naamini kwa ukongwe wa taasisi hii na uimara, tutarudi kwenye ubora wetu, matokeo haya yamemuumiza kila mtu, yamemuumiza mwalimu, benchi la ufundi, wachezaji na viongozi, lakini kwa kauli moja lazima tukubali ukweli, matokeo haya yanaweza kuikumba timu yoyote"

"Nyakati hizi zinapima watu uimara, wanachama na mashabiki wa Yanga wanatakiwa kuwa watulivu, tujiandae kwa mchezo unaofuata ili kurudi kwenye reli. Tunahitaji pointi 12 zilizobaki kusonga mbele, tunaamini tunaweza kuzipata kama tutajipanga," aliongeza Kamwe

Kikosi cha Yanga kimerejea nchini leo wakiwa na takribani siku tatu za kujiandaa kabla ya kuelekea Lubumbashi ambako wanakabiliwa na mchezo dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa Disemba 14

Yanga inahitaji ushindi au hata matokeo ya sare katika mchezo huo kabla ya timu hizo kurudiana jijini Dar es salaam wiki mbili baadae katika mchezo mwingine ambao Yanga itahitaji kushinda

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’