Wachezaji wote tunaitaka mechi - Job

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Dec 2024
Wachezaji wote tunaitaka mechi - Job

Nahodha Msaidizi wa Yanga Dickson Job amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger yanakwenda vizuri wachezaji wakiwa na ari, morali kubwa kuelekeaa mchezo huo ambao utapigwa kesho Jumamosi

Yanga ilitua Algiers juzi na jana usiku ilianza maandalizi ambapo leo watafanya mazoezi yao ya mwisho katika uwanja wa Julai 05 1962 ambao mchezo huo utapigwa hapo kesho

"Mazoezi yanaendelea vizuri sana, kuna morali kubwa kwa kila mchezaji, kesho (leo) tutafanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo utakaopigwa Jumamosi naamini tutapata matokeo mazuri katika mchezo huo"

"Morali na ari ya wachezaji iko kila mmoja anajituma kuona anapata nafasi ya kuipigania nembo ya Yanga katika mchezo huo. Hiyo ni picha nzuri kwa timu inyotaka mafanikio kwani naamini ari hii tuliyonayo mazoezini tutakwenda nayo hadi kwenye mechi"

"Tunaamini mechi itakuwa ngumu, hapa tumeshakuja mara mbili na tunafahamu jinsi mechi zinavyokuwa ukicheza katika nchi hii kwa hiyo sisi wachezaji tumejiandaa kisaikolojia na tuko tayari kupambana ili kupata matokeo mazuri"]

"Tunawaomba Wananchi ambao wako nyumbani watuombee dua, sisi vijana wao tuko tayari, tunawaahidi tutapambana ili kuweza kupata matokeo mazuri," alisema Job

Kikosi cha kocha Sead Ramovic jana usiku kilifanya mazoezi ya kwanza tangu walipotua nchini humo juzi na leo mazoezi yatahitimishwa kwenye uwanja wa July 05 1962

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’