FT : Namungo Fc 0-2 Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Nov 2024
FT : Namungo Fc 0-2 Yanga, NBC PL

Yanga imezoa alama zote tatu mkoani Lindi wakiichapa Namungo Fc mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Majaliwa, Ruangwa

Mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Kennedy Musonda na Pacome Zouzoua, yalitosha kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu katika mchezo ambao Yanga ilihitaji kushnda

Vijana wa Kocha Sead Ramovic waliingia katika mchezo huo wakiwa na ari ya kusaka ushindi, ilikuwa ni suala la muda tu Yanga kufunga baada ya kwenda mapumziko matokeo yakiwa suluhu ya bila kufungana

Namungo walishindwa kuhimili kasi ya Yanga katika kipindi cha pili, Kennedy Musonda akifunga bao la kwanza dakika ya 50 akimalizia pasi ya Maxi Nzengeli kabla ya Pacome kufunga la pili dakika ya 67 akimalizia pasi ya Clatous Chama aliyeingia kuchukua nafasi ya Aziz Ki

Alama tatu muhimu kwa Yanga ambazo zinarejesha ari ya ushindi kwa kikosi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’