Tuna deni kwa mashabiki wetu - Ramovic

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Nov 2024
Tuna deni kwa mashabiki wetu - Ramovic

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amewashukuru mashabiki waliosafiri kwa wingi kutoka jijini Dar es salaam na maeneo mengine kuelekea Ruangwa kuiunga mkono Yanga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Majaliwa

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Ramovic amesema ni deni kubwa kwao kuhakikisha wanawapa furaha mashabiki wao kwa kushinda mchezo huo

Zaidi ya mabasi 7 yanaondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea Ruangwa kuipa sapoti Yanga katika mchezo huo

"Kwakweli ni jambo la Kujivunia sana, Nawashukuru sana mashabiki wa Yanga wanaotoka Dar es Salaam leo usiku na Wanayanga Wote wanaokuja Kuisapoti timu yetu hapo kesho, mimi na Wachezaji wangu tunapaswa kuwalipa Furaha, Wameonesha Moyo na Mapenzi ya Dhati, tunajiandaa kuirejesha furaha yao," alisema Ramovic

Akizungumzia maandalizi ya kikosi Ramovic amesema wako tayari na wanachohitaji ni kushinda mchezo huo unaotarajiwa kuwa mgumu

"Tuna mchezo mgumu na muhimu sana hapo kesho, katika maandalizi yetu mpaka sasa kila kitu kipo vizuri, tunafahamu Namungo wana wachezaji wazoefu lakini sisi hatupo hapa kutafuta kingine zaidi ya alama tatu," alisema

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, Denis Nkane amesema wanakwenda kwenye mechi hii huku wakifahamu deni walilonalo baada ya kupoteza mechi zilizopita

"Sisi kama Wachezaji tunatambua umuhimu wa alama tatu kwenye Ligi, tumekaa chini na kuzungumza wapi kwa Kuboresha, tunamsikiliza Mwalimu na kujituma kwa dhati ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri, mchezo wa kesho ni mgumu lakini tupo kwaajili ya Kupambana na kushinda"

"Kwanza niwapongeze Wanayanga kwa mapenzi wanayoonesha, Nimesikia Leo wanasafiri kutoka maeneo mbalimbali na kuja kutusapoti, hili ni deni kwetu na tunapaswa Kulilipa, niwaombe Wanayanga wa Ruangwa nao waje kutusapoti kesho, tupo hapa kwa ajili ya kushinda," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’