Mshambuliaji Jean Baleke ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga walioondoka mapema leo kuelekea Ruangwa mkoani Lindi kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc
Yanga itaumana na Namungo Fc Novemba 30 katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Majaliwa
Baleke hakuwa sehemu ya kikosi kilichopoteza mchezo wa kwanza hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal juzi Jumanne
Kuna uwezekano mkubwa kocha Sead Ramovic akamtumia katika mchezo dhidi ya Namungo, lengo likiwa kuboresha eneo la safu ya ushambuliaji
Licha ya kutopata nafasi mara kwa mara katika kikosi cha kwanza, Baleke ana bao moja katika ligi kuu ya NBC
Kumekuwa na shauku kutoka kwa mashabiki wa Yanga kuona mshambuliaji huyo anapewa nafasi zaidi hasa katika kipindi hiki ambacho Yanga bado inaonekana kujitafuta katika safu ya ushambuliaji
Ramovic hakufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na kikosi chake katika mchezo uliopita pengine haitashangaza kuona mabadiliko ya kikosi katika mchezo ujao
Farid Mussa aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu nae amejumuishwa katika kikosi kilichosafiri mapema leo