Mwamnyeto awaalika mashabiki kwa Mkapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Nov 2024
Mwamnyeto awaalika mashabiki kwa Mkapa

Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa hapo kesho katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Hilal

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Mwamnyeto amesema wamejiandaa kuwapa furaha mashabiki wao kwa kushinda mchezo huo

Baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo kwenye ligi kuu ya NBC, Mwamnyeto amewahakikishia Wananchi kuwa mchezo wa kesho utakuwa tofauti, wafike kwa wingi dimba la Mkapa kushuhudia burudani

"Matokeo ya mechi zilizopita ni mechi za Ligi, sasa hivi tunakwenda kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, niwaombe mashabiki waondoe hofu na waje kwa wingi uwanjani. Tusahau yaliopita na kesho tuanze safari nyingine"

"Kwa muda mchache tuliokaa na mwalimu yako mambo ametupa na tumeyaelewa, kesho naamini mtakuja kuona mpira tofauti na ladha ya tofauti kutoka kwetu"

"Tunaelewa mechi itakuwa ngumu, lakini sisi tumejiandaa vizuri na ninaamini tutakwenda kupambana kwa ajili ya timu yetu na mashabiki wetu. Niwaombe mashabiki waje kwa wingi na kutushangilia kwa dakika zote 90 tutakazokuwa tunapambana uwanjani," alisema Mwamnyeto

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
45m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’