Mashabiki wa Yanga wameendelea kukata tiketi kwa wingi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa Jumanne, Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Maafisa wa Yanga leo wameendesha kampeni kubwa ya hamasa jijini Dar es salaam ambapo wakazi wa maeneo ya Kawe, Buguruni na Kivukoni walifikiwa na maafisa wa kukatisha tiketi katika maeneo yao
Ni wazi Wananchi huenda wakazimaliza tiketi mapema kabla ya siku ya Jumanne zikiwa zimesalia siku nne
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka wale ambao bado hawajakata tiketi, kutumia siku ya kesho kukata tiketi zao kwani muda hauko upande wao







ADVERTISE HERE