Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wanahitaji kuanza vyema hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kwa kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Al Hilal utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumanne Novemba 26
Kamwe amesema msimu huu malengo ni kukata tiketi ya hatua ya robo fainali mapema ili kuondokana na mazingira ya kuombea matokeo mabaya wapinzani wako ili uweze kufuzu
"Sisi kama jicho tunamtazama kwa sasa Al Hilal basi ni jicho la roho mbaya tu, hatuna msalia mtume siku ya Jumanne, hatukumalizana naye vizuri kwahiyo tuna Kisasi naye"
"Mechi zetu mbili za mwisho za Ligi ndiyo zinampa wakati mgumu Al Hilal. Ramovic ametambulisha Mfumo unaitwa Gusa Achia Twende Kwao hakika Utawapa Mechi ngumu sana Wapinzani wetu, hivyo Wananchi tuendelee kukata Tiketi tukatazame Soka la Kijerumani"
"Safari hii hatutamani kabisa zile hesabu za kuomba fulani afungwe ili tufuzu, mnakumbuka msimu uliyopita hatukuanza vizuri mechi yetu ya kwanza kule Algeria. Niwambie Wanayanga wote safari hii tunapaswa kuchukua pointi 3 kwenye mechi zote za nyumbani, hivyo basi tunawahitaji sana Uwanjani siku hiyo," alisema Kamwe
Akizungumzia hamasa iliyozinduliwa leo kuelekea mchezo huo, Kamwe amesema watatumia njia mbalimbali katika kuwahamasisha mashabiki wajitokeze kwa wingi siku ya Jumanne
"Yapo makundi matatu ambayo ningependa kuwaambia kuwa tushiriki kwa Pamoja kwenye Mchezo wetu dhidi ya Al Hilal. Kundi la Kwanza ni Magroup yote ya Yanga ya Whatsap, Tumekubaliana nao kuwa kwenye Hamasa hizi kusiwe na habari zozote kwenye magroup yao zaidi ya Habari za Kukata tiketi tu"
"Kila Member ahakikishe amekata tiketi ndiyo atapewa ruhusa ya Kuchat, Kundi la Pili ni Wanavyuo,Niwaombe Wanafunzi wote wa Vyuo, Walimu na Viongozi, tunawahitaji sana Siku ya Jumanne kwakuwa sote tunatambua kuwa Yanga ndiyo timu ya Vijana na ina wanachama wengi Mavyuoni, kwahiyo Njooni tuandike historia hii kwa pamoja"
"Kundi la Tatu ni Ndugu zangu wa Bodaboda, Siku hii kutakuwa na Route nyingi sana, kwahiyo tunaomba wazingatie Usalama wa Abiria wao lakini pia Wasiendeshe Siku Nzima, Ikifika saa 10 wanatakiwa kupaki boda boda zao waingie Uwanjani, Tumezungumza hapa kuwa Tiketi Zikatwe na Watu waje Uwanjani," alisema Kamwe