Kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Jumanne, Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, leo Yanga inaanza kampeni maalum ya kuhamasisha mashabiki kueleke mchezo huo
Malengo ni kuhakikisha uwanja wa Benjamin Mkapa unakuwa 'full house' katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ataongoza timu ya hamasa ambapo zoezi hilo litaanza saa 2 asubuhi
Wananchi wanaendelea kuhamasishwa kununua tiketi ambapo kuna kila dalili tiketi zitamalizika kabla ya siku ya mchezo, Jumanne
ADVERTISE HERE