Ramovic kuanza kazi ya kuisuka upya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Nov 2024
Ramovic kuanza kazi ya kuisuka upya Yanga

Baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki, kikosi cha Yanga leo kinarejea mazoezini kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Jumanne, Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kikosi leo kinarejea mazoezini kikiwa na mabadiliko ya benchi la ufundi ambapo itakuwa siku ya kwanza kazini kwa Kocha Mkuu Sead Ramovic pamoja na kocha msaidizi anayesubiri kutambulishwa sambamba na Abdihamid Moallin aliyekuwa kocha wa KMC ambaye huenda akapewa majukumu mapya ya Mkurugenzi wa ufundi

Kocha aliyesitishiwa mkataba Miguel Gamondi alisimamia mazoezi ya kikosi wiki iliyopita hadi siku ya Alhamisi pale uongozi ulipofikia uamuzi wa kusitisha mkataba wake na kumtangaza Ramovic aliyetua kutoka klabu ya TS Galaxy ya Afrika Kusini

Baada ya kutambulishwa, Ramovic hakuwa na muda wa kupoteza kwani mwishoni mwa wiki alifanya vikao na uongozi pamoja na benchi la ufundi pia akipata nafasi ya kuifahamu Yanga kwa undani ikiwa ni pamoja na kutazama mechi mbalimbali ambazo Yanga imecheza msimu huu

Kocha huyo raia wa Ujerumani atakuwa na wiki moja ya kukiandaa kikosi chake kabla ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Jumanne, Novemba 26

Ujio wa kocha mpya unatoa nafasi kwa kila mchezaji kupambania nafasi yake katika kikosi. Haitakuwa ajabu kuona baadhi ya wachezaji ambao walikuwa hawapati nafasi enzi za kocha Gamondi kuwashuhudia wakicheza mbele ya Ramovic

Ramovic anaonekana ni kocha asiye na masihara, ameweka msimamo wake mapema kuwa katika kikosi chake hataki wachezaji wavivu wa mazoezi, walevi na wale wanaopenda 'kujirusha' nyakati za usiku

Ramovic anafundisha soka la Kijerumani ambalo linahitaji nguvu, kasi na 'fitness' ya wachezaji kuwa juu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
4m ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
4h ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Toure ameweka kambani kila raundi CAFCL
Toure ameweka kambani kila raundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Ipo namna Manqoba anafelishwa na tmu yake
Ipo namna Manqoba anafelishwa na tmu yake
1d ago
READ MORE β†’
Kangwanda alihitaji dakika 15 kudhihirisha ubora wake
Kangwanda alihitaji dakika 15 kudhihirisha ubora wake
1d ago
READ MORE β†’