Bao la Kennedy Musonda liliihakikishia kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ivory Coast jana na kufuzu kwa michuano ya Afcon 2025
Musonda ameendeleza kasi ya kuzifumania nyavu akiwa na timu ya Taifa ya Zambia, akifunga mabao matatu katika hatua ya makundi
Naye mlinda lango Djigui Diarra akaiongoza Mali kupata ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Msumbaji na kukata tiketi ya kufuzu kwa michuano hiyo wakiwa na mechi mmoja mkononi
Prince Dube akiwa na timu ya Taifa ya Zimbabwe jana walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Kenya ambayo kiungo wa Yanga Duke Abuya alikuwa sehemu ya kikosi
Matokeo hayo yakaihakikishia Zimbabwe kufuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika mwakani nchini Morocco
Burkina Faso, Uganda, Zambia, Mali na Zimbabwe zimefuzu kwa michuano hiyo na pengine nyota wa Yanga Stephane Aziz Ki, Khalid Aucho, Kennedy Musonda, Clatous Chama, Djigui Diarra na Prince Dube tutawashuhudia 'mbashara' nchini Morocco mwakani