Daktari wa Yanga Moses Etutu amesema mlinzi wa kulia Yao Kouassi amerejea kikosini baada ya kupona malaria
Etutu amesema Yao yuko fit na ameungana na wachezaji wenzake katika maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Novemba 26
Hata hivyo Etutu amebainisha kuwa Yanga itaendelea kuwakosa Chedrack Boka na Aziz Andambwile ambao wanaendelea kutibiwa changamoto za majeraha
"Yao yuko imara sasa, alikuwa na homa iliyomfanya akosekane katika mechi zilizopita. Ameanza mazoezi na wenzake na tunatarajia atakuwa tayari kutumika katika mechi zijazo"
"Bado tuna majeruhi wengine Chadrack Boka na Aziz Andambwile ambao wanaendelea na program za matibabu"
"Andambwile anaweza kurejea baada ya siku 10 na Boka tunatarajia baada ya wiki atakuwa amepona na tayari kurudi kikosini," alisema Etutu
Β Nyota hao wanaweza kuwahi mchezo dhidi ya Al Hilal, ukiwa mchezo wa kwanza hatua ya makundi ligi ya mabingwa utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa