Hii ndio sababu kwa nini Yanga inahitaji kushinda Jumapili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Apr 2018
Hii ndio sababu kwa nini Yanga inahitaji kushinda Jumapili
Yanga inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom ikiwa na alama 48, hizo ni alama 11 nyuma ya Simba inayoongoza ligi na alama 59.

Hata hivyo Yanga ina michezo miwili ya kiporo ambayo kama itafanikiwa kushinda yote kimahesabu itaweza kuwa na alama 54.

Kama Yanga itaifunga Simba keshokutwa basi itaweza kupunguza zaidi tofauti kati yao hadi alama mbili. Lakini ni lazima ishinde michezo yake ya kiporo pia.

Yakitokea mazingira hayo huenda michezo ya lala salama ndio ikaamua hatma ya ubingwa msimu huu.

Mchezo wa mwisho Yanga itakuwa uwanja wa Taifa kuikabili Azam FC wakati Simba itakuwa Songea kuikabili Majimaji.

Baada ya mchezo dhidi ya Simba, Yanga itabaki na michezo sita dhidi ya Mbao FC (H), Mtibwa Sugar (A), Mwadui FC (A), Prisons (A), Ruvu Shooting (H) na Azam FC (H)

Wakati Simba itabaki na michezo minne dhidi ya Ndanda FC (H), Singida United (A), Kagera Sugar (H) na Majimaji (A)

Sababu nyingine inayoifanya Yanga isake ushindi kwa namna yoyote kwenye mchezo huo ni kurejesha HESHIMA mahali pake.

Mwaka huu Yanga imekumbwa na changamoto ambazo kwa kiasi kikubwa zimevuruga sehemu kubwa ya mipango yake.

Lakini, licha ya changamoto hizo, wachezaji wamekuwa wakijituma.

Kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika halikuwa jambo dogo na kwa kiasi kikubwa limeongeza ari ya wachezaji.

Heshima ya Yanga kuwa ndiyo wafalme wa soka la Tanzania itarejeshwa na ushindi keshokutwa.

Hii inatokana na mazingira.

Wakati huu Yanga imekuwa 'ikipuuuzwa' kwamba msimu huu haina kitu wakati wapinzani wake Simba wakionekana kama timu bora zaidi.

Ushindi kwenye mazingira haya ambayo bila shaka hata mashabiki wa Simba wataingia uwanjani na matokeo yao mfukoni utaipaisha zaidi Yanga.

Matokeo ya sare au kufungwa sio aina ya matokeo ambayo Yanga inahitaji kwenye mchezo dhidi ya Simba Jumapili.

Kipigo kitaiondoa rasmi Yanga kwenye kinyan'ganyiro cha ubingwa wakati matokeo ya sare yatafifisha zaidi matumaini ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo

Hii ndio sababu kwa nini April 29 ni siku ya kumshikisha adabu mtani!
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’