Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewapongeza mashabiki wa timu hiyo kwa uungwana waliowaonyesha wachezaji wao jana baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United
Licha ya kupoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 3-1 katika uwanja wa Azam Complex, mashabiki walibaki uwanjani hadi filimbi ya mwisho na walisimama kuwapigia makofi wachezaji wao wakati wakitoka uwanjani
Imezoeleka kwa timu nyingi hapa nchini zinapopoteza mchezo hufikia hatua hata ya kuwarushia wachezaji wao makopo ya maji, kuwazomea na kuwatukana
Mashabiki wa Yanga walionyesha mfano wa ustaarabu na kukubali matokeo pale mambo yanapokuwa sio mazuri upande wako
"Nawapenda Wananchi, kama msemaji wenu naomba niseme najivunia sana nyie na ninawapenda sana"
"Tukio mlilolifanya jana wakati mechi ikimalizika na kupoteza mchezo LIMEWAWEKA KWENYE DARAJA LA JUU MNO. Limeonyesha Ukomavu wenu kwenye mpira wa miguu na ni kwa Kiasi gani MNAIPENDA SANA TIMU YENU"
"Nataka niwaambie kitu Wananchi. Kama kuna ujumbe mkubwa mmeutuma kwa Uongozi/Bechi la Ufundi na wachezaji wetu tangu msimu huu umeanza basi ni hili tukio la jana"
"Majibu ya hii meseji yenu mtayapata kwenye mchezo dhidi ya Al Hilal," aliandika Kamwe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii