Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United
Majira ya saa 12 jioni, Yanga itakuwa mwenyeji wa Tabora United katika mchezo ambao ushindi kwa Yanga utawarudisha kileleni mwa msimamo wa ligi
Kamwe amesema wananchi focus yao iwe mchezo huo na wasikubali kuyumbishwa na propaganda zinazoanzishwa ili kuwavuruga
"Kuna propaganda zinanzishwa lengo lake ni kututoa kwenye focus ya mchezo wa leo dhidi ya Tabora United"
"Hili Haliwezi kufanikiwa, hii klabu inajua hatua zake na tuko makini. Tunakwenda kwa nguvu Kubwa leo kusaka pointi tatu"
"Akili yetu kwa sasa ni kurudi juu ya msimamo wa ligi, kata tiketi yako mapema Mwananchi," alisema Kamwe
Ushindi wa aina yoyote kwa Yanga katika mchezo huo, utatosha kuwarejesha Wananchi kileleni mwa msimamo