Baada ya kubeba tuzo ya nyota wa mchezo dhidi ya JKT Tanzania dimba la Azam Complex, juzi Profesa Pacome Zouzoua akachukua tuzo yake ya pili katika mchezo dhidi ya Singida Black Stars uliopigwa visiwani Zanzibar
Pacome alifunga katika mechi hizo mbili lakini bao alilofunga juzi lilikuwa bora zaidi na pengine linaweza kuingia katika tuzo za goli bora la msimu
Unaweza kusema Zouzoua sasa yuko katika ubora ambao Wananchi walimshuhudia msimu uliopita kabla ya kupata majeraha yaliyomuweka nje muda mrefu
Msimu huu pia hakuanza na kasi lakini kiwango alichoonyesha katika mechi tatu zilizopita dhidi ya JKT Tanzania, Coastal Union na Singida BS, kinadhihrisha Profesa amerejea
Hii ni habari njema kwa Wananchi kuelekea mchezo wa kwanza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa baadae mwezi huu
Pacome alijenga jina lake katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita, ilikuwa bahati mbaya majeraha yalimfanya akose mechi ya robo fainali dhidi ya Mamelodi