Yanga imemaliza mechi dhidi ya Singida Black Stars kwa ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana
Wananchi wameondoka Zanzibar kurejea Dar es salaam tayari kwa mchezo unaofuata dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumamosi, Novemba 02 katika uwanja wa Azam Complex
Wananchi wanasema ni mwendo wa 'kutegua mabomu' yaliyotegwa njiani
Kabla ya kuanza safari ya kurejea Dar, kikosi cha Yanga kilifanya mazoezi ya 'recovery' kwani muda wa maandalizi umekuwa mdogo




