Matchday; Singida BS vs Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Oct 2024
Matchday; Singida BS vs Yanga, NBC PL

Ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mchezo mmoja utapigwa visiwani Zanzibar katika uwanja wa New Amaan Complex

Ni mchezo utakaozikutanisha timu mbili zilizojuu katika msimamo wa ligi, Singida Black Stars dhidi ya Yanga

Singida Black Stars watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 2:30 usiku

Kikosi cha Yanga kiliwasili Zanzibar mapema jana na usiku wakafanya mazoezi yao ya mwisho katika uwanja wa New Amaan Complex

Ni wazi itakuwa mechi ngumu itakayozikutanisha timu mbili bora zaidi kwenye ligi msimu huu

Singida BS wako kileleni mwa msimamo wa ligi wakikusanya alama 22 baada ya mechi nane, hawajapoteza mchezo, wakishinda mechi 7 na kutoka sare mechi moja

Wanakutana na Yanga ambayo ina rekodi ya ushindi wa asilimia 100 bila ya kuruhusu bao

Licha ya kukiri vijana wake wanakabiliwa na uchovu baada ya kucheza mechi 7 katika siku 21, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wanakwenda katika mchezo huo wakiwa na dhamira ya kusaka ushindi

Gamondi alisema anafahamu Singida BS wana timu nzuri lakini anaamini katika mbinu, ubora wa kikosi chake kumpa nafasi ya kushinda mchezo huo

Yanga SC Stories

Yanga Princess bado haijajipata
Yanga Princess bado haijajipata
17m ago
READ MORE β†’
Pacome sasa anatembea bila magongo
Pacome sasa anatembea bila magongo
3h ago
READ MORE β†’
Manqoba katika maandalizi ya dabi ya pili
Manqoba katika maandalizi ya dabi ya pili
6h ago
READ MORE β†’
Mzize anaitaka dabi Oktoba 10
Mzize anaitaka dabi Oktoba 10
9h ago
READ MORE β†’
Kangwanda anauwasha moto Zambia
Kangwanda anauwasha moto Zambia
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 30 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 30 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya Kariakoo Derby
Maandalizi ya Kariakoo Derby
1d ago
READ MORE β†’
Edna Lema apania kumaliza uteja dhidi ya Simba Queens
Edna Lema apania kumaliza uteja dhidi ya Simba Queens
1d ago
READ MORE β†’
Familia ya Mzee Mpili yatoa shukrani kwa uongozi Yanga
Familia ya Mzee Mpili yatoa shukrani kwa uongozi Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Zokouane, Shalulile uso kwa uso kufuzu Afcon 2027 leo
Zokouane, Shalulile uso kwa uso kufuzu Afcon 2027 leo
1d ago
READ MORE β†’