Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wako ugenini mkoani Arusha kumenyana na Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Mechi nyingine ngumu ugenini kwa Wananchi wakisaka alama tatu ili kuendeleza rekodi ya ushindi wa asilimia 100 msimu huu
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amekiri hawatakuwa na mechi rahisi mbele ya Coastal Union lakini watapambana ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi
Wakati Coastal Union wakipata takribani wiki nzima ya maandalizi, hali ilikuwa tofauti kwa Yanga ambayo tangu Jumamosi iliyopita, imeshuka dimbani kila baada ya siku tatu
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki wa timu hiyo kutumia akiba zao za fedha kwenda uwanjani kuipa sapoti timu yao
Kiingilio cha chini Mzunguuko ni Tsh 10,000/- wakati VVIP ni Tsh 50,000/-, VIP A na B ni Tsh 30,000/- na VIP C ni Tsh 20,000/-
Kamwe amesema Coastal Union wamelenga kupata pesa katika mchezo huo lakini Yanga imelenga kupata alama tatu