Ziko nyakati ngumu ambazo Yanga ilipita miaka ya nyuma lakini Wananchi hawakufika hatua ya kutishia kuhama ligi
Baada ya vipigo mfululizo, Simba wamefika hatua ya kuiomba TFF imtenganishe GSM na Yanga eti anadhamini zaidi ya timu moja katika ligi, bila ya kujali kanuni zinaruhusu ama la
Wanatisha waamuzi na kutishia kuhama ligi, hizi ni kauli za watu waliokata tamaa ambao hawana matumaini
Kinachotokea sasa ni dalili za soka la Tanzania kukomaa maana zile njia za mkato kupata mafanikio zimefungwa
Siri ya kuwa na mafanikio kwa timu mpira wa miguu ni uwekezaji katika kikosi, mengine ni ziada
Timu bora inahitaji wachezaji wazuri, benchi bora la ufundi, vifaa na kambi nzuri ya maandalizi, uongozi bora na maslahi mazuri
Yanga imefanikiwa katika yote hayo na itaendelea kutawala soka la Tanzania kama wengine hawatafuata mkondo huo na kuacha ujanja ujanja na propaganda
Pongezi kwa Rais wa Yanga Injinia Hersi Said na uongozi kwa ujumla kwa kuiweka Yanga katika mfumo sahihi wa uendeshaji wa timu ya mpira wa miguu
GSM ndio sababu ya haya yote yanayotokea leo, alihakikisha Yanga inapata kila ilichohitaji. Amesimamia 'transformation', amefanikisha usajili na kuajiri benchi bora la ufundi
GSM hana maneno mengi, vitendo vinazungumza! zaidi atakuambia YANGA BINGWA...!