Klabu ya Yanga imeamuliwa na FIFA kuwalipa wachezaji Augustine Okrah na Hafidh Konkoni baada ya wachezaji hao kushinda kesi za madai ya kuvunjiwa mikataba yao
Yanga iliachana na wachezaji hao raia wa Ghana baada ya kutoridhishwa na viwango vyao
Baadhi ya mashabiki wanaweza kutupia lawama uongozi wa Yanga kwa kesi hizi ambazo wanaamini zinachafua 'brand' ya klabu
Lakini kwa upande mwingine hiyo ndio gharama ya kujenga kikosi imara
Uongozi wa Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said, umeweka wazi kuwa kila mchezaji ana jukumu la kuipambania nafasi yake na kuisaidia timu kufikia malengo
Kama mchezaji anashindwa kutimiza wajibu wake, ataondoka na nafasi yake atapewa mchezaji mwingine ambaye yuko tayari kupambana
Unapozungumzia uimara wa kikosi cha Yanga, pamoja na kazi nzuri inayofanywa na benchi la ufundi, wachezaji wanajitoa sana kwani wanafahamu kama hawatafanya vizuri basi safari itawakuta wakati wowote
Madeni ni sehemu ya maisha ya Taasisi kubwa kote duniani, kama Yanga ingeogopa kuvunja mikataba ya wachezaji wasiokidhi mahitaji kwa kuogopa madeni, pengine leo isingekuwa na ubora huu
Mashabiki wa Yanga hawapaswi kuingia katika mtego wa propaganda kila inapokuja mechi kubwa, deni sio kitu cha ajabu