Yanga yaja na mkakati wa kupunguza 'fatique' kwa wachezaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Oct 2024
Yanga yaja na mkakati wa kupunguza 'fatique' kwa wachezaji

Katika kuhakikisha wachezaji wake wanarejea haraka ili kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya mechi ya dabi, mabosi wa Yanga wameandaa utaratibu wa kuwarejesha mapema nyota waliokuwa kwenye timu za mataifa yao, imefahamika

Mechi ya watani wa jadi ya mzunguko wa kwanza ambayo Simba watakuwa wenyeji itachezwa Oktoba 19, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amesema wameandaa utaratibu wa kuhakikisha wachezaji wao wote wanarudi nchini haraka na kwa njia rahisi, ili kujiepusha na uchovu wa kusafiri kwa muda mrefu

"Idara yetu ya utimamu kwa mwili imekuwa ikifanya mawasiliano na wachezaji wote kuhakikisha wanalinda miili yao na tunaangalia njia zote rahisi na nzuri kuhakikisha wanarudi mapema na salama, ili kuuwahi mchezo huo, wakiwa hawana uchovu"

"Changamoto kubwa ambayo wachezaji wanaipata ni kusafiri, ukiangalia taratibu za kuunganisha safari za ndege kwenye jiografia ya bara la Afrika, mchezaji anatakiwa akae njiani kwa siku mbili, atoke nchi moja ya Afrika, aende mpaka Ulaya (Uturuki), akae saa 10 au 15 na pengine mpaka 20, halafu arejee tena Afrika, hii inafanya wachezaji kuwa na mchoko au fatiki, akifika badala ya kupumzika anatakiwa ajiandae na mchezo unaofuata wa klabu yake," alisema Kamwe

Aliongeza hata makocha wanavyolalamika juu ya wachezaji wao kwenda kwenye vikosi vya timu za taifa, mara nyingi huwa ni usafiri na si kucheza mechi nyingi kwa muda mfupi

"Waliopanga ratiba si watu ambao hawajui mpira, wapo sahihi kabisa, kila kitu kimepangwa ndani ya kanuni za soka na taratibu zake. Taratibu zinasema mchezaji anatakiwa kukaa saa 72 kabla ya kucheza mchezo mwingine, tatizo kubwa siku zote huwa ni usafiri tu, safari hii sisi tumeliangalia," Kamwe alisema

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’