Viungo wa Yanga Khalid Aucho na Clatous Chama jana walikuwa na majukumu ya kuziongoza timu zao za Taifa katika mechi za kuwania kufuzu Afcon 2025
Chama alivaa kitambaa cha unahodha katika mchezo dhidi ya Chad uliopigwa Zambia na kumalizika kwa matokeo ya suluhu yaa bila kufungana
Mshambuliaji Kennedy Musonda alicheza dakika zote 90 za mchezo huo ambao licha ya Zambia kukosa alama zote tatu, imesalia katika nafasi ya pili kundi S ikiwa na alama nne

Aucho akiwa nahodha wa Uganda, aliiongoza timu hiyo kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sudan Kusini katika mchezo uliopigwa dimba la Namboole, Uganda
Huo ulikuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Uganda ambayo iko kileleni mwa kundi K ikiwa na alama 7 sawa na Afrika Kusini
Haikuwa siku nzuri kwa Duke Abuya na timu ya Taifa ya Kenya wakikubali kipigo cha mabao 4-1 ugenini huko Cameroon. Abuya alikuwa sehemu ya kikosi cha Kenya kilichoanza mchezo huo