Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze ametua klabu ya Kaizer Chiefs kuungana na Nasreddine Nabi kama kocha msaidizi
Kaze na Nabi walikuwa na mafanikio makubwa katika misimu miwili waliyofanya kazi pamoja Yanga wakishinda mataji mawili ya ligi kuu, kombe la FA na Ngao ya Jamii pia wakiisaidia Yanga kucheza fainali ya kombe la Shirikisho la CAF (CAF CC)
Baada ya Nabi kutua Kaizer Chiefs, alipendekeza kwa klabu hiyo kumuajiri Kaze katika majukumu ya kocha msaidizi akiamini katika uwezo wake
Benchi la ufundi la Kaizer Chiefs sasa litakuwa na takribani makocha wanne ambao walifanya kazi pamoja Yanga
Chiefs iko katika jitihada za kusukwa upya baada ya kupotea kwenye ramani ya soka la Afrika Kusini na Kimataifa kwa misimu kadhaa
Wakati wa pre-season kuelekea msimu huu waliialika Yanga katika mchezo maalum wa Toyota Cup, Yanga ikibeba kombe baada ya ushindi wa mabao 4-0
Chiefs na Yanga zimefungua ushirikiano katika masuala mbalimbali ya kimpira